Masharti na Kanuni
Kamwene Festival 2026 · 27 & 28 Novemba 2026 · Viwanja vya Chuo Kikuu cha Mkwawa, Iringa
Zimeandaliwa na JuaKali Events Company Limited ·
Zimehuishwa 29.09.2026
1. Usajili na malipo
- Usajili unakamilika pale malipo yanapopokelewa. Utapewa namba ya kumbukumbu na tiketi yenye QR.
- Ada ya usajili hairudishwi. Kama huwezi kushiriki, unaweza kumpa mtu mwingine nafasi yako kwa kutuarifu kabla ya tarehe 20 Novemba 2026.
- Tiketi ni ya mshiriki aliyetajwa. Namba ya kumbukumbu isishirikishwe hadharani.
2. Umri
- Mbio za watoto (km 1.5) ni kwa watoto wenye umri chini ya miaka 13. Mzazi au mlezi lazima awepo.
- Mshiriki mwenye umri chini ya miaka 18 anahitaji ridhaa ya mzazi au mlezi, ambaye ndiye anayejisajili kwa niaba yake.
3. Afya na usalama
- Kwa kujisajili unathibitisha kuwa una afya njema ya kushiriki katika umbali ulioukchagua, na unashiriki kwa hiari yako mwenyewe.
- Fuata maelekezo ya waratibu na askari wa njia muda wote. Waratibu wanaweza kumtoa mshiriki yeyote kwa sababu za usalama.
- Huduma ya kwanza itapatikana siku ya tukio. JuaKali Events Company Limited haiwajibiki kwa majeraha, upotevu au uharibifu, isipokuwa pale sheria inapoelekeza vinginevyo.
4. Picha na video
- Tukio hili litapigwa picha na kurekodiwa video. Kwa kushiriki, unaruhusu JuaKali Events Company Limited na washirika wake kutumia picha na video zenye sura yako katika matangazo, mitandao ya kijamii, tovuti, magazeti na machapisho mengine, bila malipo.
- Ruhusa hii haina mwisho wa muda na inahusu matumizi ya tukio hili na matangazo ya matukio yajayo.
- Kama hutaki picha yako itumike, tuambie kabla ya tukio kwa kamwene@juakalievents.co.tz, au utuandikie ili tuondoe picha husika. Tutaheshimu ombi lako kwa matumizi yajayo.
- Picha za watoto: mzazi au mlezi anayejisajili kwa niaba ya mtoto ndiye anayetoa ruhusa hii.
5. Taarifa zako binafsi
- Taarifa tunazokusanya ni jina, namba ya simu, barua pepe (ukitoa), mji, umbali uliochagua na saizi ya fulana.
- Tunazitumia kwa usajili, malipo, kukutumia tiketi na taarifa za tukio pekee. Hatuziuzi wala kuzitoa kwa matangazo ya wengine.
- Malipo yanashughulikiwa na Selcom, ambaye hupokea namba yako ya simu na kiasi cha malipo ili kukamilisha muamala.
- Una haki ya kuomba nakala ya taarifa zako, kuzirekebisha au kuzifuta baada ya tukio. Wasiliana nasi kwa kamwene@juakalievents.co.tz.
6. Mabadiliko ya tukio
- Waratibu wanaweza kubadilisha ratiba, njia au muda kwa sababu za usalama, hali ya hewa au maelekezo ya mamlaka.
- Tukio likiahirishwa, usajili wako utahamishiwa kwenye tarehe mpya.
7. Kuchukua kit
- Onesha tiketi yako (QR au namba ya kumbukumbu) pamoja na kitambulisho ukija kuchukua kit yako.
- Fulana hutolewa kulingana na saizi uliyochagua wakati wa usajili, kadri zinavyopatikana.
8. Mawasiliano
- JuaKali Events Company Limited · kamwene@juakalievents.co.tz
· 0793 859 784